Kwa nini NiKao ipo
Biashara nyingi zina bidhaa au huduma nzuri lakini zinapata changamoto kujua zitangaze wapi, zitumie kiasi gani, ziwafikie watu gani na zipimeje kama matangazo yameleta wateja halisi. NiKao imejengwa kurahisisha mchakato huo.
NiKao ni jukwaa la market acquisition, advertising na conversion linalosaidia biashara kufikia watu sahihi, kutumia budget kwa uangalifu na kupima matokeo kutoka sehemu moja.
Biashara nyingi zina bidhaa au huduma nzuri lakini zinapata changamoto kujua zitangaze wapi, zitumie kiasi gani, ziwafikie watu gani na zipimeje kama matangazo yameleta wateja halisi. NiKao imejengwa kurahisisha mchakato huo.
NiKao inaunganisha campaign planning, geo targeting, budget intelligence, creative generation, lead acquisition, customer conversations, conversion tracking na campaign optimization kwenye workspace moja.
NiKao imeundwa kuanzia mazingira halisi ya biashara za Tanzania, ikiwa na uwezo wa kampeni kuanzia eneo la karibu, wilaya na mkoa hadi Tanzania nzima na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Lengo ni kufanya customer acquisition iwe rahisi kueleweka, kupimika na kufikiwa hata na biashara ndogo inayotaka kuanza na budget ndogo kama TZS 2,000 kwa siku.